Hasheem Thabeet jina la kwanza la Mtanzania kuingia kwenye Headlines Duniani akitajwa kama Mbongo wa kwanza kuchezea Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani, NBA.
Sim Bhullar unaambiwa ni jina jingine kubwa TENA kuingia kwenye NBA.. Jamaa hatokei BONGO, ni raia wa Canada ambaye tayari kasaini contract ya siku 10 na timu ya Sacramento Kings.. wazazi wake wana asili ya India, baadae walihamia Canada ambapo Bhullar alizaliwa mwaka 1992, hivyo anakuwa mchezaji wa kwanza ambaye ana asili ya India kuchezea Ligi ya NBA.
Bhullar ana urefu wa futi 7.5, anakuwa mchezaji wa kwanza kwa urefu kwa sasa hivi, anampita Hasheem Thabeet ambaye ana futi 7.3.

0 Comments